Mathayo 15:13 - Swahili Revised Union Version Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini yeye akawajibu, “Kila mmea ambao Baba yangu aliye mbinguni hakupanda, utangolewa. Biblia Habari Njema - BHND Lakini yeye akawajibu, “Kila mmea ambao Baba yangu aliye mbinguni hakupanda, utangolewa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini yeye akawajibu, “Kila mmea ambao Baba yangu aliye mbinguni hakupanda, utang'olewa. Neno: Bibilia Takatifu Akawajibu, “Kila mmea ambao Baba yangu wa mbinguni hakuupanda utang’olewa. Neno: Maandiko Matakatifu Akawajibu, “Kila pando ambalo Baba yangu wa mbinguni hakulipanda, litang’olewa. BIBLIA KISWAHILI Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa. |
Watu wako nao watakuwa wenye haki wote, Nao watairithi nchi milele; Wao ni chipukizi nililolipanda mimi mwenyewe, Kazi ya mikono yangu mwenyewe, Ili mimi nitukuzwe.
kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.
Ndipo wanafunzi wake walipomwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa?
Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.
Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.
Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung'olewa kabisa;