Mathayo 14:35 - Swahili Revised Union Version Na watu wa mahali pale walipomtambua, walituma watu kwenda nchi zile zilizo kandokando, wakamletea wote waliokuwa wagonjwa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa huko walipomtambua, wakaeneza habari pote katika sehemu hizo. Basi, wakamletea Yesu wagonjwa wote, Biblia Habari Njema - BHND Watu wa huko walipomtambua, wakaeneza habari pote katika sehemu hizo. Basi, wakamletea Yesu wagonjwa wote, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa huko walipomtambua, wakaeneza habari pote katika sehemu hizo. Basi, wakamletea Yesu wagonjwa wote, Neno: Bibilia Takatifu Watu wa eneo lile walipomtambua Isa, walipeleka habari sehemu zote za jirani. Watu wakamletea wagonjwa wao wote, Neno: Maandiko Matakatifu Watu wa eneo lile walipomtambua Isa, walipeleka habari sehemu zote za jirani. Watu wakamletea wagonjwa wao wote, BIBLIA KISWAHILI Na watu wa mahali pale walipomtambua, walituma watu kwenda nchi zile zilizo kandokando, wakamletea wote waliokuwa wagonjwa; |
wakaenda mbio, wakizunguka nchi ile yote, wakaanza kuwachukua vitandani waliokuwa wagonjwa, kwenda kila mahali waliposikia kwamba yupo.
Alipoitambua sauti ya Petro, hakulifungua lango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani akawaambia kwamba Petro anasimama mbele ya lango.
Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye mlango wa hekalu uitwao Mzuri; wakawa na mshangao na kustaajabia mambo yale yaliyompata.