Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.
Matendo 5:22 - Swahili Revised Union Version Wakati watumishi walipofika hawakuwaona gerezani, wakarudi wakatoa habari, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini hao watumishi walipofika huko hawakuwakuta mle gerezani. Hivyo walirudi, wakatoa taarifa mkutanoni, Biblia Habari Njema - BHND Lakini hao watumishi walipofika huko hawakuwakuta mle gerezani. Hivyo walirudi, wakatoa taarifa mkutanoni, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini hao watumishi walipofika huko hawakuwakuta mle gerezani. Hivyo walirudi, wakatoa taarifa mkutanoni, Neno: Bibilia Takatifu Lakini wale walinzi wa Hekalu walipoenda gerezani hawakuwakuta mitume mle. Kwa hiyo wakarudi na kutoa habari. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wale walinzi wa Hekalu walipokwenda gerezani hawakuwakuta mitume mle. Kwa hiyo wakarudi na kutoa habari. BIBLIA KISWAHILI Wakati watumishi walipofika hawakuwaona gerezani, wakarudi wakatoa habari, |
Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.
wakisema, Gereza tumeikuta imefungwa salama, nao walinzi wamesimama mbele ya mlango; lakini tulipoufungua hatukukuta mtu ndani.
Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga kwa mawe.