Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
Matendo 19:11 - Swahili Revised Union Version Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu alifanya miujiza ya ajabu kwa mikono ya Paulo. Biblia Habari Njema - BHND Mungu alifanya miujiza ya ajabu kwa mikono ya Paulo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu alifanya miujiza ya ajabu kwa mikono ya Paulo. Neno: Bibilia Takatifu Mungu akafanya miujiza mingi isiyo ya kawaida kupitia kwa Paulo, Neno: Maandiko Matakatifu Mungu akafanya miujiza mingi isiyo ya kawaida kwa mkono wa Paulo, BIBLIA KISWAHILI Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida; |
Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
Basi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa ushujaa katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao.
Basi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa.
Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.
Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;
Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.
Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?
Mungu naye akishuhudia pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.