Hasira ya Balaki ikawaka juu ya Balaamu akayapiga makofi; Balaki akamwambia Balaamu, Nilikuita ili unilaanie adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa mara tatu hizi.
Matendo 11:10 - Swahili Revised Union Version Jambo hili likatendeka mara tatu, kisha vitu vyote vikavutwa tena juu mbinguni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jambo hilo lilifanyika mara tatu, na mwishowe vyote vilirudishwa juu mbinguni. Biblia Habari Njema - BHND Jambo hilo lilifanyika mara tatu, na mwishowe vyote vilirudishwa juu mbinguni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jambo hilo lilifanyika mara tatu, na mwishowe vyote vilirudishwa juu mbinguni. Neno: Bibilia Takatifu Jambo hili lilitokea mara tatu, ndipo kile kitu kikavutwa tena mbinguni. Neno: Maandiko Matakatifu Jambo hili lilitokea mara tatu, ndipo kile kitu kikavutwa tena mbinguni. BIBLIA KISWAHILI Jambo hili likatendeka mara tatu, kisha vitu vyote vikavutwa tena juu mbinguni. |
Hasira ya Balaki ikawaka juu ya Balaamu akayapiga makofi; Balaki akamwambia Balaamu, Nilikuita ili unilaanie adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa mara tatu hizi.
Yesu akamjibu, Je! Wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia, Jogoo hatawika hadi wewe utakapokuwa umenikana mara tatu.
Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
Na tazama, mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba tuliyokuwamo, waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria.
Sauti ikanijibu mara ya pili kutoka mbinguni, Alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najisi.