Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.
Matendo 10:26 - Swahili Revised Union Version Lakini Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwanadamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Petro alimwinua, akamwambia, “Simama, kwa maana mimi ni binadamu tu.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini Petro alimwinua, akamwambia, “Simama, kwa maana mimi ni binadamu tu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Petro alimwinua, akamwambia, “Simama, kwa maana mimi ni binadamu tu.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini Petro akamwinua akamwambia, “Simama, mimi ni mwanadamu tu.” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Petro akamwinua akamwambia, “Simama, mimi ni mwanadamu tu.” BIBLIA KISWAHILI Lakini Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwanadamu. |
Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.
Naam, mkono wangu umeuweka msingi wa dunia, na mkono wangu wa kulia umezitanda mbingu; niziitapo husimama pamoja.
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.
Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mtumishi mwenzako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.