Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uangamizao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?
Marko 9:44 - Swahili Revised Union Version ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.] Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Humo, wadudu wake hawafi na moto hauzimiki.] Biblia Habari Njema - BHND Humo, wadudu wake hawafi na moto hauzimiki.] Neno: Bibilia Takatifu Ni mahali ambako funza wao hawafi wala moto wao hauzimiki.] Neno: Maandiko Matakatifu Mahali ambako funza wake hawafi wala moto wake hauzimiki.] BIBLIA KISWAHILI ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.] |
Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uangamizao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?
Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
Kisha atawaambia na wale walioko katika mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa kibutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako Jehanamu, kwenye moto usiozimika; [
Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, ukiwa kiguru, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika Jehanamu; [
watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;
yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-kondoo.
Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.