Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
Marko 2:18 - Swahili Revised Union Version Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwa nini wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati mmoja wanafunzi wa Yohane na wanafunzi wa Mafarisayo walikuwa wanafunga. Basi, watu wakaja, wakamwuliza Yesu, “Kwa nini wanafunzi wa Yohane na wa Mafarisayo wanafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?” Biblia Habari Njema - BHND Wakati mmoja wanafunzi wa Yohane na wanafunzi wa Mafarisayo walikuwa wanafunga. Basi, watu wakaja, wakamwuliza Yesu, “Kwa nini wanafunzi wa Yohane na wa Mafarisayo wanafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati mmoja wanafunzi wa Yohane na wanafunzi wa Mafarisayo walikuwa wanafunga. Basi, watu wakaja, wakamwuliza Yesu, “Kwa nini wanafunzi wa Yohane na wa Mafarisayo wanafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?” Neno: Bibilia Takatifu Basi wanafunzi wa Yahya pamoja na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Watu wakamjia Isa na kumuuliza, “Mbona wanafunzi wa Yahya na wa Mafarisayo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?” Neno: Maandiko Matakatifu Basi wanafunzi wa Yahya pamoja na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Baadhi ya watu wakamjia Isa na kumuuliza, “Mbona wanafunzi wa Yahya na wa Mafarisayo hufunga lakini wanafunzi wako hawafungi?” BIBLIA KISWAHILI Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwa nini wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi? |
Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana arusi pamoja nao hawawezi kufunga.
Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.