Marko 11:10 - Swahili Revised Union Version umebarikiwa na ufalme ujao, wa baba yetu Daudi. Hosana juu mbinguni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ubarikiwe ufalme ujao wa baba yetu Daudi. Sifa kwa Mungu juu mbinguni!” Biblia Habari Njema - BHND Ubarikiwe ufalme ujao wa baba yetu Daudi. Sifa kwa Mungu juu mbinguni!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ubarikiwe ufalme ujao wa baba yetu Daudi. Sifa kwa Mungu juu mbinguni!” Neno: Bibilia Takatifu “Umebarikiwa ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi!” “Hosana kwake yeye aliye juu!” Neno: Maandiko Matakatifu “Umebarikiwa Ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi!” “Hosana kwake yeye aliye juu!” BIBLIA KISWAHILI umebarikiwa na ufalme ujao, wa baba yetu Daudi. Hosana juu mbinguni. |
ndipo nitawatupilia mbali wazao wa Yakobo, na Daudi, mtumishi wangu, hata nisitwae wazao wake watawale juu ya wazao wa Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; kwa maana nitawarudisha wafungwa wao, nami nitawarehemu.
baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta BWANA, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea BWANA na wema wake kwa kicho siku za mwisho.
Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Abrahamu watoto.