BWANA asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu.
Marko 10:4 - Swahili Revised Union Version Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nao wakasema, “Mose aliagiza mume kumpatia mkewe hati ya talaka na kumwacha.” Biblia Habari Njema - BHND Nao wakasema, “Mose aliagiza mume kumpatia mkewe hati ya talaka na kumwacha.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nao wakasema, “Mose aliagiza mume kumpatia mkewe hati ya talaka na kumwacha.” Neno: Bibilia Takatifu Wakajibu, “Musa aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.” Neno: Maandiko Matakatifu Wakajibu, “Musa aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.” BIBLIA KISWAHILI Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha. |
BWANA asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu.
Watu husema, Mtu akimwacha mkewe, naye akienda zake, akawa mke wa mtu mwingine, je! Mtu huyo atamrudia tena? Je! Nchi hiyo haitatiwa unajisi? Lakini wewe umefanya mambo ya ukahaba na wapenzi wengi; nawe, je! Utanirudia mimi? Asema BWANA.
Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.