Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu.
Marko 1:39 - Swahili Revised Union Version Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, akaenda kila mahali huko Galilaya akihubiri katika masunagogi na kufukuza pepo. Biblia Habari Njema - BHND Basi, akaenda kila mahali huko Galilaya akihubiri katika masunagogi na kufukuza pepo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, akaenda kila mahali huko Galilaya akihubiri katika masunagogi na kufukuza pepo. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo akazunguka Galilaya yote, akihubiri katika masinagogi yao na kutoa pepo wachafu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo akazunguka Galilaya kote, akihubiri katika masinagogi yao na kutoa pepo wachafu. BIBLIA KISWAHILI Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo. |
Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu.
Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha.
Akawaambia, Twendeni mahali pengine, katika vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana nilikuja kwa ajili ya hilo.
Akastaajabu kwa sababu ya kutoamini kwao. Akazungukazunguka katika vile vijiji, akifundisha.
Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka.
Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye Kristo.