Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako?
Marko 1:25 - Swahili Revised Union Version Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akamkemea huyo pepo akisema, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” Biblia Habari Njema - BHND Yesu akamkemea huyo pepo akisema, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akamkemea huyo pepo akisema, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini Isa akamkemea, akamwamuru, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu!” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Isa akamkemea, akamwambia, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!” BIBLIA KISWAHILI Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke. |
Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako?
Macho yao yakafumbuka. Naye Yesu akawaagiza kwa nguvu, akisema, Angalieni hata mtu mmoja asijue.
Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.
Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena.
Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, mtoke. Ndipo yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka pasipo kumdhuru.
Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye Kristo.
Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.