Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Marko 1:13 - Swahili Revised Union Version

Akawako huko jangwani siku arubaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwituni, na malaika walikuwa wakimhudumia.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

akakaa huko siku arubaini akijaribiwa na Shetani. Alikuwa huko pamoja na wanyama wa porini, nao malaika wakawa wanamhudumia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

akakaa huko siku arubaini akijaribiwa na Shetani. Alikuwa huko pamoja na wanyama wa porini, nao malaika wakawa wanamhudumia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

akakaa huko siku arubaini akijaribiwa na Shetani. Alikuwa huko pamoja na wanyama wa porini, nao malaika wakawa wanamhudumia.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

naye Isa akawa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikaa na wanyama pori, nao malaika wakamhudumia.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

naye akawa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikaa na wanyama wa mwituni, nao malaika wakamhudumia.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwituni, na malaika walikuwa wakimhudumia.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Marko 1:13
13 Marejeleo ya Msalaba  

Musa akaingia ndani ya lile wingu, akapanda mlimani; Musa akawa humo katika ule mlima siku arubaini, mchana na usiku.


Naye alikuwa huko pamoja na BWANA siku arubaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi.


Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?


Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.


Na Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho kwa muda wa siku arubaini nyikani,


Ikawa mwisho wa siku arubaini usiku na mchana, BWANA alinipa zile mbao mbili za mawe, nazo ni mbao za agano.


Nikaanguka chini mbele za BWANA siku arubaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyofanya, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kwa kumkasirisha.


Ndipo nikaanguka chini mbele za BWANA siku zile arubaini usiku na mchana nilizokuwa nimeanguka chini; kwa kuwa BWANA alisema atawaangamiza.


Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.


Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa kama sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.