Uwape sawasawa na vitendo vyao, Na kwa kadiri ya uovu wa matendo yao, Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao, Uwalipe kile wanachostahili.
Maombolezo 3:64 - Swahili Revised Union Version Utawalipa malipo, Ee BWANA, Sawasawa na kazi ya mikono yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uwalipize, ee Mwenyezi-Mungu kadiri ya hayo matendo yao, kadiri ya mambo waliyotenda wenyewe. Biblia Habari Njema - BHND Uwalipize, ee Mwenyezi-Mungu kadiri ya hayo matendo yao, kadiri ya mambo waliyotenda wenyewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uwalipize, ee Mwenyezi-Mungu kadiri ya hayo matendo yao, kadiri ya mambo waliyotenda wenyewe. Neno: Bibilia Takatifu Uwalipe kile wanachostahili, Ee Mwenyezi Mungu, kwa yale ambayo mikono yao imetenda. Neno: Maandiko Matakatifu Uwalipe kile wanachostahili, Ee bwana, kwa yale ambayo mikono yao imetenda. BIBLIA KISWAHILI Utawalipa malipo, Ee BWANA, Sawasawa na kazi ya mikono yao. |
Uwape sawasawa na vitendo vyao, Na kwa kadiri ya uovu wa matendo yao, Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao, Uwalipe kile wanachostahili.
Lakini, Ee BWANA wa majeshi, uhukumuye haki, ujaribuye fikira na moyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.
Ee BWANA, unajua wewe; unikumbuke, unijie, ukanilipizie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na matukano.
Waiteni wapiga mishale juu ya Babeli, Naam, wote waupindao upinde; Pangeni hema kumzunguka pande zote; Ili asiokoke hata mtu mmoja wao; Mlipeni kwa kadiri ya kazi yake; Mtendeni sawasawa na yote aliyoyatenda; Kwa sababu amefanya kiburi juu ya BWANA, Juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.
Nami nitamlipa Babeli, na wote wakaao ndani ya Ukaldayo, mabaya yao yote, waliyoyatenda katika Sayuni mbele ya macho yenu, asema BWANA.
Kwa maana mwenye kuangamiza amefika kwake; Naam, amefika Babeli; Na mashujaa wake wametwaliwa; Pinde zao zimevunjika kabisa; Maana BWANA ni Mungu wa kisasi; Hakika yake yeye atalipa.
Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo.
Iskanda, mfua shaba, alionesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa kulingana na matendo yake.
Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni mara mbili.
Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, na Mkweli, utakawia hadi lini kuhukumu na kuilipa damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?