Maombolezo 3:46 - Swahili Revised Union Version Juu yetu adui zetu wote Wametupanulia vinywa vyao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Maadui zetu wote wanatuzomea. Biblia Habari Njema - BHND “Maadui zetu wote wanatuzomea. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Maadui zetu wote wanatuzomea. Neno: Bibilia Takatifu “Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyao wazi dhidi yetu. Neno: Maandiko Matakatifu “Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyao wazi dhidi yetu. BIBLIA KISWAHILI Juu yetu adui zetu wote Wametupanulia vinywa vyao. |
Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya moyo wangu.
Kwa nini mataifa yaseme, Yuko wapi Mungu wao? Kisasi cha damu ya watumishi wako iliyomwagika Kijulike kati ya mataifa machoni petu.
Lakini katika wana wa Israeli hapana hata mbwa atakayetoa ulimi juu yao, juu ya mtu wala juu ya mnyama; ili kwamba mpate kujua jinsi BWANA anavyowatenga Wamisri na Waisraeli.
Juu yako adui zako wote Wamepanua vinywa vyao; Huzomea, husaga meno yao, Husema, Tumemmeza; Hakika siku hii ndiyo tuliyoitazamia; Tumeipata, tumeiona.