Na vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa kwa vidogo, na hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za mfalme, na za wakuu wake; vyote pia akavileta Babeli.
Maombolezo 1:10 - Swahili Revised Union Version Huyo mtesi amenyosha mkono wake Juu ya matamanio yake yote; Maana ameona ya kuwa mataifa wameingia Ndani ya patakatifu pake; Ambao kwa habari zao wewe uliamuru Wasiingie katika kusanyiko lako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maadui wamenyosha mikono yao, wanyakue vitu vyake vyote vya thamani. Naam umeona watu wa mataifa wakiingia hekaluni, watu ambao Mwenyezi-Mungu aliwakataza kujumuika na jumuiya ya watu wake. Biblia Habari Njema - BHND Maadui wamenyosha mikono yao, wanyakue vitu vyake vyote vya thamani. Naam umeona watu wa mataifa wakiingia hekaluni, watu ambao Mwenyezi-Mungu aliwakataza kujumuika na jumuiya ya watu wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maadui wamenyosha mikono yao, wanyakue vitu vyake vyote vya thamani. Naam umeona watu wa mataifa wakiingia hekaluni, watu ambao Mwenyezi-Mungu aliwakataza kujumuika na jumuiya ya watu wake. Neno: Bibilia Takatifu Adui ametia mikono juu ya hazina zake zote, aliona mataifa ya kipagani wakiingia mahali patakatifu pake, wale uliowakataza kuingia kwenye kusanyiko lako. Neno: Maandiko Matakatifu Adui ametia mikono juu ya hazina zake zote, aliona mataifa ya kipagani wakiingia mahali patakatifu pake, wale uliowakataza kuingia kwenye kusanyiko lako. BIBLIA KISWAHILI Huyo mtesi amenyosha mkono wake Juu ya matamanio yake yote; Maana ameona ya kuwa mataifa wameingia Ndani ya patakatifu pake; Ambao kwa habari zao wewe uliamuru Wasiingie katika kusanyiko lako. |
Na vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa kwa vidogo, na hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za mfalme, na za wakuu wake; vyote pia akavileta Babeli.
Siku hiyo walisoma katika kitabu cha Musa masikioni mwa watu; na ndani yake yalionekana maneno haya yameandikwa, ya kwamba Mwamoni na Mmoabi wasiingie katika kusanyiko la Mungu milele;
Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako.
Mali yako na hazina zako nitazitoa kuwa nyara, bila kulipwa thamani yake; naam, kwa sababu ya dhambi zako zote, hata katika mipaka yako yote.
Tena mali zote za mji huu, na mapato yake yote, na vitu vyake vya thamani vyote pia, naam, hazina zote za wafalme wa Yuda, nitavitia katika mikono ya adui zao, watakaowateka nyara, na kuwakamata, na kuwachukua mpaka Babeli.
Maana BWANA wa majeshi asema hivi, kuhusu habari za nguzo, na kuhusu habari za bahari, na kuhusu habari za vilingo vyake, na kuhusu habari za mabaki ya vyombo vilivyoachwa katika mji huu,
naam, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, katika habari za vyombo vilivyobaki katika nyumba ya BWANA, na katika nyumba ya mfalme wa Yuda, na hapa Yerusalemu;
Sauti yao wakimbiao na kuokoka, Kutoka katika nchi ya Babeli, Ili kutangaza katika Sayuni kisasi cha BWANA, Mungu wetu, Kisasi cha hekalu lake.
Twaona haya kwa kuwa tumesikia shutuma; Fedheha imetufunika nyuso zetu; Kwa sababu wageni wamepaingia Patakatifu pa nyumba ya BWANA.
Akaiteketeza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto.
Siku za mateso na misiba yake, Yerusalemu huyakumbuka matamanio yake yote Yaliyokuwa tangu siku za kale; Hapo watu wake walipoanguka mikononi mwa mtesi, Wala hakuna hata mmoja wa kumsaidia; Hao watesi wake walimwona, Wakafanya sabato zake kuwa mzaha.
kuwa mmewaingiza wageni, ambao mioyo yao haikutahiriwa, wala miili yao haikutahiriwa, wawe ndani ya patakatifu pangu, wapatie unajisi, naam, nyumba yangu, mtoapo sadaka ya chakula changu, mafuta na damu; nao wameyavunja maagano yangu, juu ya machukizo yenu yote.
Tena nitaugeuza uso wangu usiwaelekee, nao watapatia unajisi mahali pangu pa siri; na wanyang'anyi wataingia humo na kupatia unajisi.
Akawaambia, itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa; haya, nendeni. Wakaenenda, wakaua watu katika mji.
Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Yudea na wakimbilie milimani;
Mwamoni wala Mmoabi wasiingie katika mkutano wa BWANA; wala hata kizazi cha kumi mtu wao asiingie katika mkutano wa BWANA milele;
kwa sababu hapo mlipotoka Misri hawakuwalaki na chakula wala maji njiani; na kwa kuwa walimwajiri juu yako Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyo Mesopotamia, aje akuapize.