Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotayarishwa.
Luka 9:30 - Swahili Revised Union Version Na tazama, watu wawili walikuwa wakizungumza naye, nao ni Musa na Eliya; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Na watu wawili wakaonekana wakizungumza naye, nao walikuwa Mose na Elia, Biblia Habari Njema - BHND Na watu wawili wakaonekana wakizungumza naye, nao walikuwa Mose na Elia, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Na watu wawili wakaonekana wakizungumza naye, nao walikuwa Mose na Elia, Neno: Bibilia Takatifu Ghafula wakawaona watu wawili, ndio Musa na Ilya, wakizungumza naye. Neno: Maandiko Matakatifu Ghafula wakawaona watu wawili, ndio Musa na Ilya, wakizungumza naye. BIBLIA KISWAHILI Na tazama, watu wawili walikuwa wakizungumza naye, nao ni Musa na Eliya; |
Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotayarishwa.
Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa ningali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika vitabu vya Manabii na Zaburi.
Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine, Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.
Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta.
walioonekana katika utukufu, wakanena habari za kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemu.
Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.