Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
Luka 4:21 - Swahili Revised Union Version Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye akaanza kuwaambia, “Andiko hili mlilosikia limetimia leo.” Biblia Habari Njema - BHND Naye akaanza kuwaambia, “Andiko hili mlilosikia limetimia leo.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye akaanza kuwaambia, “Andiko hili mlilosikia limetimia leo.” Neno: Bibilia Takatifu Ndipo akaanza kwa kuwaambia, “Leo andiko hili limetimia mkiwa mnasikia.” Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo akaanza kwa kuwaambia, “Leo Andiko hili limetimia mkiwa mnasikia.” BIBLIA KISWAHILI Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. |
Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
Akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?
Mnayachunguza maandiko kwa sababu mnadhani kuwa ndani yake ninyi mna uzima wa milele; na maandiko yayo hayo ndiyo yanayonishuhudia.
Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo.