Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.
Luka 4:15 - Swahili Revised Union Version Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye akawa anawafundisha watu katika masunagogi yao, akasifiwa na wote. Biblia Habari Njema - BHND Naye akawa anawafundisha watu katika masunagogi yao, akasifiwa na wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye akawa anawafundisha watu katika masunagogi yao, akasifiwa na wote. Neno: Bibilia Takatifu Akaanza kufundisha kwenye masinagogi yao, na kila mmoja akamsifu. Neno: Maandiko Matakatifu Akaanza kufundisha kwenye masinagogi yao, na kila mmoja akamsifu. BIBLIA KISWAHILI Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote. |
Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.
Na alipofika mji wa kwao, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?
Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu.
Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii.
Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii!
Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini waziwazi; bali alikaa nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila upande.
Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.