Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.
Luka 24:51 - Swahili Revised Union Version Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni. Biblia Habari Njema - BHND Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni. Neno: Bibilia Takatifu Alipokuwa anawabariki, akawaacha, akachukuliwa mbinguni. Neno: Maandiko Matakatifu Alipokuwa anawabariki, akawaacha, akachukuliwa mbinguni. BIBLIA KISWAHILI Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni. |
Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.
Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kulia wa Mungu.
Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.
Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.
Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na chapa kamili ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi katika mkono wa kulia wa Ukuu huko juu;
Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.