Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto wa kiume, naye atamwita jina lake Imanueli.
Luka 20:44 - Swahili Revised Union Version Basi Daudi amwita Bwana; amekuwaje mwana wake? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ikiwa Daudi anamwita yeye, ‘Bwana,’ basi, atakuwaje mwanawe?” Biblia Habari Njema - BHND Ikiwa Daudi anamwita yeye, ‘Bwana,’ basi, atakuwaje mwanawe?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ikiwa Daudi anamwita yeye, ‘Bwana,’ basi, atakuwaje mwanawe?” Neno: Bibilia Takatifu Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?” Neno: Maandiko Matakatifu Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?” BIBLIA KISWAHILI Basi Daudi amwita Bwana; amekuwaje mwana wake? |
Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto wa kiume, naye atamwita jina lake Imanueli.
Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.
Lakini ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzawa wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.