Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Luka 20:37 - Swahili Revised Union Version Lakini, ya kuwa wafu hufufuliwa, hata na Musa alionesha katika sura ya Kichaka, hapo alipomtaja Bwana kuwa ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka kwa wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo. Biblia Habari Njema - BHND Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka kwa wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka kwa wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo. Neno: Bibilia Takatifu Hata Musa alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila kuteketea, alipomwita Mwenyezi Mungu, ‘Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.’ Neno: Maandiko Matakatifu Hata Musa alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila kuteketea, alipomwita Bwana Mwenyezi Mungu, ‘Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.’ BIBLIA KISWAHILI Lakini, ya kuwa wafu hufufuliwa, hata na Musa alionesha katika sura ya Kichaka, hapo alipomtaja Bwana kuwa ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. |
Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Abrahamu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii unayolala nitakupa wewe na uzao wako.
Yakobo akasema, Ee Mungu wa baba yangu Abrahamu, na Mungu wa baba yangu Isaka, BWANA, uliyeniambia, Rudi uende mpaka nchi yako, na kwa jamaa zako, nami nitakutendea mema;
Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.
Na kwa vitu vilivyo bora vya nchi, na kujaa kwake, Na uradhi wake aliyekaa ndani ya kile kichaka; Na ije baraka juu ya kichwa chake Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliyetengwa na nduguze.