Palikuwa na mji mdogo, uliokuwa na watu wachache ndani yake; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga.
Luka 19:43 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana siku zaja ambapo adui zako watakuzungushia maboma, watakuzingira na kukusonga pande zote. Biblia Habari Njema - BHND Maana siku zaja ambapo adui zako watakuzungushia maboma, watakuzingira na kukusonga pande zote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana siku zaja ambapo adui zako watakuzungushia maboma, watakuzingira na kukusonga pande zote. Neno: Bibilia Takatifu Hakika siku zinakujia, ambazo adui zako watakuzingira, nao watakuzunguka pande zote na kukuzuilia ndani. Neno: Maandiko Matakatifu Hakika siku zinakujia, ambazo adui zako watakuzingira, nao watakuzunguka pande zote na kukuzuilia ndani. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; |
Palikuwa na mji mdogo, uliokuwa na watu wachache ndani yake; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga.
Basi, BWANA asema hivi kuhusu mfalme wa Ashuru, Yeye hataingia ndani ya mji huu, wala hatapiga mshale hapa, wala hatakuja mbele yake kwa ngao, wala hatajenga boma juu yake.
Atawaua binti zako kwa upanga katika mashamba; naye atafanya ngome juu yako, na kufanya maboma juu yako, na kuiinua ngao juu yako.
ukauhusuru, ukajenge ngome juu yake, na kufanya boma juu yake; ukaweke makambi juu yake, na kuweka magogo ya kuubomoa yauzunguke pande zote.
Basi yule mfalme akaghadhibika; akatuma majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.
akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.