Luka 13:12 - Swahili Revised Union Version Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umeponywa ugonjwa wako.” Biblia Habari Njema - BHND Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umeponywa ugonjwa wako.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umeponywa ugonjwa wako.” Neno: Bibilia Takatifu Isa alipomwona, akamwita, akamwambia, “Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako.” Neno: Maandiko Matakatifu Isa alipomwona, akamwita, akamwambia, “Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako.” BIBLIA KISWAHILI Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. |
Watu wasionitaka wanauliza habari zangu; nimeonekana na hao wasionitafuta; nililiambia taifa lisiloitwa kwa jina langu,
Yafueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari.
Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu.
Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa wagonjwa,
Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.
Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Abrahamu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato?