Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliujua ule wakati mwizi atakaokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
Luka 12:38 - Swahili Revised Union Version Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata kama atarudi usiku wa manane au alfajiri na kuwakuta wanakesha, heri yao watumishi hao! Biblia Habari Njema - BHND Hata kama atarudi usiku wa manane au alfajiri na kuwakuta wanakesha, heri yao watumishi hao! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata kama atarudi usiku wa manane au alfajiri na kuwakuta wanakesha, heri yao watumishi hao! Neno: Bibilia Takatifu Itakuwa heri kwa watumwa hao ikiwa bwana wao atakapokuja atawakuta wamekesha hata kama atakuja usiku wa manane, au karibu na mapambazuko. Neno: Maandiko Matakatifu Itakuwa heri kwa watumwa hao ikiwa bwana wao atakapokuja atawakuta wamekesha hata kama atakuja mnamo usiku wa manane, au karibu na mapambazuko. BIBLIA KISWAHILI Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao. |
Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliujua ule wakati mwizi atakaokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
Lakini fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua saa atakayokuja mwizi, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa.