Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao liko katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,
Luka 12:13 - Swahili Revised Union Version Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mmoja katika ule umati wa watu akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu tugawane urithi aliotuachia baba.” Biblia Habari Njema - BHND Mtu mmoja katika ule umati wa watu akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu tugawane urithi aliotuachia baba.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mmoja katika ule umati wa watu akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu tugawane urithi aliotuachia baba.” Neno: Bibilia Takatifu Mtu mmoja katika umati ule wa watu akamwambia Isa, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu tugawane naye urithi wetu.” Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mmoja katika umati wa watu akamwambia Isa, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu tugawane naye urithi wetu.” BIBLIA KISWAHILI Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu. |
Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao liko katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,
Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao.
Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
na kuzozana miongoni mwa watu waliopotoka katika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.