Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.
Luka 12:10 - Swahili Revised Union Version Na kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Mtu atasamehewa, bali aliyemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Yeyote anayesema neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa; lakini anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. Biblia Habari Njema - BHND “Yeyote anayesema neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa; lakini anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Yeyote anayesema neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa; lakini anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. Neno: Bibilia Takatifu Naye kila atakayenena neno baya dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu wa Mungu hatasamehewa. Neno: Maandiko Matakatifu Naye kila atakayenena neno baya dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho wa Mwenyezi Mungu hatasamehewa. BIBLIA KISWAHILI Na kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali aliyemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. |
Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.
ingawa hapo awali nilikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye ujeuri, lakini nilipata rehema kwa kuwa nilifanya hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.
Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.