lakini BWANA, Mungu wenu, ndiye mtakayemcha; naye atawaokoa mikononi mwa adui zenu wote.
Luka 1:71 - Swahili Revised Union Version Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kwamba atatuokoa mikononi mwa maadui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia. Biblia Habari Njema - BHND kwamba atatuokoa mikononi mwa maadui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kwamba atatuokoa mikononi mwa maadui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia. Neno: Bibilia Takatifu kwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu, na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao: Neno: Maandiko Matakatifu kwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu, na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao: BIBLIA KISWAHILI Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia; |
lakini BWANA, Mungu wenu, ndiye mtakayemcha; naye atawaokoa mikononi mwa adui zenu wote.
Akawaokoa kutoka kwa mkono wa mtu adui, aliyewachukia, Na kuwakomboa kutoka kwa mkono wa adui zao.
Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa zako.
Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu.
Tazama, nitawakusanya, na kuwatoa katika nchi zote nilikowafukuza, katika hasira yangu, na uchungu wangu, na ghadhabu yangu nyingi; nami nitawaleta tena hadi mahali hapa, nami nitawakalisha salama salimini;
Nao watakaa humo salama; naam, watajenga nyumba, na kupanda mashamba ya mizabibu, na kukaa salama; nitakapokuwa nimetekeleza hukumu zangu juu ya watu wote, wanaowatenda mambo ya jeuri pande zote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao.
Nami nitafanya agano la amani nao, nami nitawakomesha wanyama wakali kati yao; nao watakaa salama jangwani, na kulala misituni.
Hawatakuwa mateka ya mataifa tena, wala mnyama wa nchi hatawala; bali watakaa salama salimini, wala hapana mtu atakayewatia hofu.
Na baada ya siku nyingi utakusanywa; katika miaka ya mwisho, utaingia nchi iliyorudishiwa hali yake ya kwanza, baada ya kupigwa kwa upanga, iliyokusanywa toka kabila nyingi za watu, juu ya milima ya Israeli, iliyokuwa ukiwa wa daima; lakini imetolewa katika makabila ya watu, nao watakaa salama salimini wote pia.
U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.
atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.