Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Luka 1:50 - Swahili Revised Union Version Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huruma yake kwa watu wanaomcha hudumu kizazi hata kizazi. Biblia Habari Njema - BHND Huruma yake kwa watu wanaomcha hudumu kizazi hata kizazi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huruma yake kwa watu wanaomcha hudumu kizazi hata kizazi. Neno: Bibilia Takatifu Rehema zake hudumu kizazi hadi kizazi, kwa wale wanaomcha. Neno: Maandiko Matakatifu Rehema zake huwaendea wale wamchao, kutoka kizazi hadi kizazi. BIBLIA KISWAHILI Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha. |
Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
lakini BWANA, Mungu wenu, ndiye mtakayemcha; naye atawaokoa mikononi mwa adui zenu wote.
Maana, kama mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Ndivyo fadhili zake zilivyo kuu kwa wamchao.
Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako Ulizowawekea wakuchao; Ulizowatendea wakukimbiliao Mbele ya wanadamu!
Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakubwa.