Luka 1:47 - Swahili Revised Union Version Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu. Biblia Habari Njema - BHND roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu. Neno: Bibilia Takatifu nayo roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu, Neno: Maandiko Matakatifu nayo roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu, BIBLIA KISWAHILI Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; |
Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.
Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na Kristo Yesu, tarajio letu;
akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliokabidhiwa kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu;
wasiwe wezi; bali wauoneshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mungu aliye Mwokozi wetu katika mambo yote.
tukilitazamia tumaini lenye baraka na kufunuliwa kwa utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina.