Luka 1:46 - Swahili Revised Union Version Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye Maria akasema, “Moyo wangu wamtukuza Bwana, Biblia Habari Njema - BHND Naye Maria akasema, “Moyo wangu wamtukuza Bwana, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye Maria akasema, “Moyo wangu wamtukuza Bwana, Neno: Bibilia Takatifu Naye Mariamu akasema: “Moyo wangu wamwadhimisha Mwenyezi Mungu, Neno: Maandiko Matakatifu Naye Mariamu akasema: “Moyo wangu wamwadhimisha Mwenyezi Mungu, BIBLIA KISWAHILI Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, |
Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.
Ila Mungu ashukuriwe, anayetufanya tushangilie ushindi daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.
Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamumwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,