Ole wa taji la kiburi la walevi wa Efraimu, na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, la hao walioshindwa na divai!
Isaya 9:8 - Swahili Revised Union Version Bwana alimpelekea Yakobo neno, nalo likamfikia Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu ametoa tamko dhidi ya Yakobo nalo litampata Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu ametoa tamko dhidi ya Yakobo nalo litampata Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu ametoa tamko dhidi ya Yakobo nalo litampata Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Bwana ametuma ujumbe dhidi ya Yakobo, utamwangukia Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Bwana ametuma ujumbe dhidi ya Yakobo, utamwangukia Israeli. BIBLIA KISWAHILI Bwana alimpelekea Yakobo neno, nalo likamfikia Israeli. |
Ole wa taji la kiburi la walevi wa Efraimu, na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, la hao walioshindwa na divai!
Mamlaka ya enzi yake yatakuzwa daima, Na kutakuwa na amani isiyo na mwisho, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
Nao watu wote watajua, yaani, Efraimu na yeye akaaye Samaria, wasemao kwa kiburi na kwa kujisifu nafsi zao,
ndipo Azaria, mwana wa Hoshaya, na Yohana mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakanena, wakimwambia Yeremia, Unasema uongo; BWANA, Mungu wetu, hakukutuma useme, Msiende Misri kukaa huko;
Lakini maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je, Hazikuwapata baba zenu? Nao wakatubu na kusema, BWANA wa majeshi ametutenda kulingana na njia zetu, na matendo yetu, kama alivyokusudia kutenda.