Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.
Isaya 9:11 - Swahili Revised Union Version Kwa sababu hiyo BWANA atawainua adui wa Resini juu yake, naye atawachochea adui zake; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Mwenyezi-Mungu atawaletea wapinzani na kuwachochea maadui zao. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Mwenyezi-Mungu atawaletea wapinzani na kuwachochea maadui zao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Mwenyezi-Mungu atawaletea wapinzani na kuwachochea maadui zao. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Mwenyezi Mungu amemtia nguvu adui wa Resini dhidi yao na kuchochea watesi wao. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini bwana amemtia nguvu adui wa Resini dhidi yao na kuchochea watesi wao. BIBLIA KISWAHILI Kwa sababu hiyo BWANA atawainua adui wa Resini juu yake, naye atawachochea adui zake; |
Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.
Na huyo mfalme wa Ashuru akamsikia; mfalme wa Ashuru akapanda juu ya Dameski, akautwaa, akawahamisha watu wake mateka mpaka Kiri, akamwua Resini.
Watainama chini ya wafungwa tu, wataanguka chini yao waliouawa. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Ole wa taji la kiburi la walevi wa Efraimu, na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, la hao walioshindwa na divai!
Kwa sababu hiyo hasira ya BWANA imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Hata ikawa katika siku za Ahazi, mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, mfalme wa Yuda, Resini, mfalme wa Shamu, na Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakapanda wakaenda Yerusalemu ili kupigana nao, lakini hawakuweza kuushinda.
Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini; na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande, asiwe kabila la watu tena;