lakini BWANA, Mungu wenu, ndiye mtakayemcha; naye atawaokoa mikononi mwa adui zenu wote.
Isaya 8:12 - Swahili Revised Union Version Msiseme, Ni njama, kuhusu mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni njama; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Usijumuike nao katika njama zao, wala usiogope yale wanayoyaogopa wala kuwa na hofu. Biblia Habari Njema - BHND “Usijumuike nao katika njama zao, wala usiogope yale wanayoyaogopa wala kuwa na hofu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Usijumuike nao katika njama zao, wala usiogope yale wanayoyaogopa wala kuwa na hofu. Neno: Bibilia Takatifu “Usiite fitina kila kitu ambacho watu hawa hukiita fitina, usiogope kile wanachokiogopa, wala usikihofu. Neno: Maandiko Matakatifu “Usiite fitina kila kitu ambacho watu hawa hukiita fitina, usiogope kile wanachokiogopa, wala usikihofu. BIBLIA KISWAHILI Msiseme, Ni njama, kuhusu mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni njama; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope. |
lakini BWANA, Mungu wenu, ndiye mtakayemcha; naye atawaokoa mikononi mwa adui zenu wote.
Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu, Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru. Umewatia aibu, Kwa sababu MUNGU amewadharau.
Ole wa watoto waasi; asema BWANA; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu; wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi;
Nanyi mtakaposikia habari za vita na fitina, msitishwe; maana, hayo hayana budi kutukia kwanza, lakini ule mwisho hauji upesi.
Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.
Basi Yoshua akakwea kutoka Gilgali, yeye, na watu wa vita wote pamoja naye, na mashujaa wote wenye uwezo.