Ikawa, Yoramu alipomwona Yehu, akasema, Je! Ni amani, Yehu? Akajibu, Amani gani, maadamu uzinzi wa mama yako Yezebeli na uchawi wake ni mwingi?
Isaya 57:21 - Swahili Revised Union Version Hapana amani kwa waovu; asema Mungu wangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu wangu asema hivi: “Watu waovu sitawapa amani.” Biblia Habari Njema - BHND Mungu wangu asema hivi: “Watu waovu sitawapa amani.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu wangu asema hivi: “Watu waovu sitawapa amani.” Neno: Bibilia Takatifu Mungu wangu asema, “Hakuna amani kwa waovu.” Neno: Maandiko Matakatifu Mungu wangu asema, “Hakuna amani kwa waovu.” BIBLIA KISWAHILI Hapana amani kwa waovu; asema Mungu wangu. |
Ikawa, Yoramu alipomwona Yehu, akasema, Je! Ni amani, Yehu? Akajibu, Amani gani, maadamu uzinzi wa mama yako Yezebeli na uchawi wake ni mwingi?
Lakini nikasema, Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina BWANA, na thawabu yangu ina Mungu wangu.
Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika mienendo yao; wamejifanyia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani.
yaani, manabii wa Israeli, watabirio habari za Yerusalemu, na kuona maono ya amani katika habari zake; wala hapana amani, asema Bwana MUNGU.