Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa; Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.
Isaya 45:16 - Swahili Revised Union Version Watatahayarika, naam, watafadhaika, wote pia; wale watengenezao sanamu wataingia fadhaa pamoja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watengenezaji sanamu wataaibika na kufadhaika, wote kwa pamoja watavurugika. Biblia Habari Njema - BHND Watengenezaji sanamu wataaibika na kufadhaika, wote kwa pamoja watavurugika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watengenezaji sanamu wataaibika na kufadhaika, wote kwa pamoja watavurugika. Neno: Bibilia Takatifu Wote watengenezao sanamu wataaibika na kutahayarika; wataenda kutahayarika pamoja. Neno: Maandiko Matakatifu Wote watengenezao sanamu wataaibika na kutahayarika; wataenda kutahayarika pamoja. BIBLIA KISWAHILI Watatahayarika, naam, watafadhaika, wote pia; wale watengenezao sanamu wataingia fadhaa pamoja. |
Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa; Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.
Nitapanda katika jangwa mwerezi, mshita, mhadasi, na mbono; nitatia katika nyika mberoshi, mtidhari, na mteashuri pamoja;
Watarudishwa nyuma, wataaibishwa sana, hao wanaotumainia sanamu za mawe, na kuziambia sanamu za madini, Ninyi ndinyi miungu yetu.
Tazama, wenziwe wote watatahayari; na mafundi, hao ni wanadamu; na wakusanyike pamoja, wakasimame; wataogopa na kutahayari pamoja.
Wachongao sanamu, wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike.
Jikusanyeni mje; na kukaribia pamoja, ninyi wa mataifa mliookoka; hawana maarifa wale wachukuao mti wa sanamu yao ya kuchonga; wamwombao mungu asiyeweza kuokoa.
Na Moabu ataona haya kwa ajili ya Kemoshi, kama nyumba ya Israeli ilivyoona haya kwa ajili ya Betheli, tegemeo lao.