Isaya 34:7 - Swahili Revised Union Version Na nyati watateremka pamoja nao, na ndama pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyati wataangamia pamoja nao, ndama kadhalika na mafahali. Nchi italoweshwa damu, udongo utarutubika kwa mafuta yao. Biblia Habari Njema - BHND Nyati wataangamia pamoja nao, ndama kadhalika na mafahali. Nchi italoweshwa damu, udongo utarutubika kwa mafuta yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyati wataangamia pamoja nao, ndama kadhalika na mafahali. Nchi italoweshwa damu, udongo utarutubika kwa mafuta yao. Neno: Bibilia Takatifu Nyati wataanguka pamoja nao, ndama dume na mafahali wakubwa. Nchi yao italowana kwa damu, nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama. Neno: Maandiko Matakatifu Nyati wataanguka pamoja nao, ndama waume na mafahali wakubwa. Nchi yao italowana kwa damu, nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama. BIBLIA KISWAHILI Na nyati watateremka pamoja nao, na ndama pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu. |
Mkemee mnyama wa mafunjoni; Kundi la mafahali, na ndama za watu; Hata wanyenyekee na kuleta vipande vya fedha, Uwatawanye watu wapendao vita.
Nikayakanyaga makabila ya watu kwa hasira yangu, Nikawalevya kwa ghadhabu yangu, Nami nikaimwaga damu yao chini.
Ombolezeni, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.
Na askari wake waliojiwa, walio kati yake, Ni kama ndama walionona malishoni; Maana wao nao wamerudi nyuma, Wamekimbia wote pamoja, wasisimame; Maana siku ya msiba wao imewafikia, Wakati wa kujiliwa kwao.
Kwa sababu mnafurahi, kwa sababu mnashangilia, enyi mnaouteka urithi wangu, kwa sababu mmenona kama mtamba akanyagaye nafaka, nanyi mnalia kama farasi wenye nguvu;
Wachinjeni mafahali wake wote; Na wateremkie machinjoni; Ole wao! Maana siku yao imewadia, Wakati wa kujiliwa kwao.
Tena kwa damu yako nitainywesha nchi, ambayo waogelea juu yake, hata milimani; na mifereji ya maji itajawa nawe.
Na wewe, mwanadamu, Bwana MUNGU asema hivi; Sema na ndege wa kila namna, na kila mnyama wa porini, Jikusanyeni, mje; jikusanyeni pande zote mwijie karamu yangu ya kafara ninayoandaa kwa ajili yenu, naam, karamu kuu ya kafara juu ya milima ya Israeli, mpate kula nyama na kunywa damu.
Mtakula nyama yao walio hodari, na kunywa damu ya wakuu wa dunia, ya kondoo dume na ya wana-kondoo, na ya mbuzi, na ya ng'ombe, wote na wanono wa Bashani.
Mungu amemleta kutoka Misri, Ana nguvu mfano wa nguvu za nyati; Atawameza mataifa walio adui zake, Ataivunja mifupa yao vipande vipande. Atawachoma kwa mishale yake.
Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase.