Isaya 24:9 - Swahili Revised Union Version Hawatakunywa divai pamoja na nyimbo; kileo kitakuwa uchungu kwao wakinywao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hakuna tena kunywa divai na kuimba; mvinyo umekuwa mchungu kwa wanywaji. Biblia Habari Njema - BHND Hakuna tena kunywa divai na kuimba; mvinyo umekuwa mchungu kwa wanywaji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hakuna tena kunywa divai na kuimba; mvinyo umekuwa mchungu kwa wanywaji. Neno: Bibilia Takatifu Hawanywi tena mvinyo pamoja na wimbo, kileo ni kichungu kwa wanywaji wake. Neno: Maandiko Matakatifu Hawanywi tena mvinyo pamoja na wimbo, kileo ni kichungu kwa wanywaji wake. BIBLIA KISWAHILI Hawatakunywa divai pamoja na nyimbo; kileo kitakuwa uchungu kwao wakinywao. |
Wewe nenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako.
Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!
Nami nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio; nami nitatia nguo za magunia katika viuno vyote, na upara katika kila kichwa; nami nitayafanya haya kuwa kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.
Tena nyimbo za hekaluni zitakuwa vilio siku ile, asema Bwana MUNGU; mizoga itakuwa mingi; kila mahali wataitupa, wakinyamaza kimya.
BWANA wa majeshi atawalinda; Nao watakula na kuyakanyaga mawe ya teo; Nao watakunywa na kufanya kelele kama kwa divai; Nao watajazwa kama mabakuli, kama pembe za madhabahu.