Na furaha imeondolewa, na shangwe toka mashamba yaliyozaa sana; hapana kuimba katika mashamba ya mizabibu, wala sauti za furaha; akanyagaye hakanyagi divai katika mashinikizo; nimeikomesha sauti ya furaha yake akanyagaye.
Isaya 24:7 - Swahili Revised Union Version Divai mpya inaomboleza, mzabibu umedhoofika, watu wote waliochangamka moyo wanaugua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mizabibu inanyauka, divai inakosekana. Wote waliokuwa wenye furaha sasa wanasononeka kwa huzuni. Biblia Habari Njema - BHND Mizabibu inanyauka, divai inakosekana. Wote waliokuwa wenye furaha sasa wanasononeka kwa huzuni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mizabibu inanyauka, divai inakosekana. Wote waliokuwa wenye furaha sasa wanasononeka kwa huzuni. Neno: Bibilia Takatifu Divai mpya inakauka na mzabibu unanyauka, watu wote wafurahishao wanalia kwa huzuni. Neno: Maandiko Matakatifu Divai mpya inakauka na mzabibu unanyauka, watu wote wafurahishao wanalia kwa huzuni. BIBLIA KISWAHILI Divai mpya inaomboleza, mzabibu umedhoofika, watu wote waliochangamka moyo wanaugua. |
Na furaha imeondolewa, na shangwe toka mashamba yaliyozaa sana; hapana kuimba katika mashamba ya mizabibu, wala sauti za furaha; akanyagaye hakanyagi divai katika mashinikizo; nimeikomesha sauti ya furaha yake akanyagaye.
Maana mashamba ya Heshboni yamenyauka, na mzabibu wa Sibma; mabwana wa mataifa wameyavunja matawi yake mateule; yamefika hadi Yazeri, yalitangatanga hadi jangwani matawi yake yalitapakaa, yaliivuka bahari.
Ndipo katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, nitaikomesha sauti ya kicheko na sauti ya furaha, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi; kwa maana nchi hiyo itakuwa ukiwa.
Nami nitanyosha mkono wangu juu yao, na kuifanya nchi kuwa maganjo, tena ukiwa mbaya kuliko jangwa upande wa Dibla, katika makao yao yote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.