Isaya 23:4 - Swahili Revised Union Version Tahayari, Ee Sidoni; kwa maana bahari imenena, hiyo ngome ya bahari ilisema, Sikuona uchungu, wala sikuzaa, wala sikulea vijana, wala sikulea wanawali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aibu kwako ewe Sidoni, mji wa ngome kando ya bahari! Bahari yenyewe yatangaza: “Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa, wala sijawahi kuzaa; sijawahi kulea wavulana, wala kutunza wasichana!” Biblia Habari Njema - BHND Aibu kwako ewe Sidoni, mji wa ngome kando ya bahari! Bahari yenyewe yatangaza: “Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa, wala sijawahi kuzaa; sijawahi kulea wavulana, wala kutunza wasichana!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aibu kwako ewe Sidoni, mji wa ngome kando ya bahari! Bahari yenyewe yatangaza: “Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa, wala sijawahi kuzaa; sijawahi kulea wavulana, wala kutunza wasichana!” Neno: Bibilia Takatifu Uaibishwe ee Sidoni, nawe ee ngome la bahari, kwa kuwa bahari imesema: “Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa wala sijapata kuzaa, wala sijapata kulea wana wala kutunza binti.” Neno: Maandiko Matakatifu Uaibishwe ee Sidoni, nawe ee ngome la bahari, kwa kuwa bahari imesema: “Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa wala sijapata kuzaa, wala sijapata kulea wana wala kutunza mabinti.” BIBLIA KISWAHILI Tahayari, Ee Sidoni; kwa maana bahari imenena, hiyo ngome ya bahari ilisema, Sikuona uchungu, wala sikuzaa, wala sikulea vijana, wala sikulea wanawali. |
Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.
na wafalme wote wa Tiro, na wafalme wote wa Sidoni, na wafalme wote wa kisiwa kilicho ng'ambo ya pili ya bahari;
kisha uvipeleke kwa mfalme wa Edomu, na mfalme wa Moabu, na mfalme wa wana wa Amoni, na mfalme wa Tiro, na mfalme wa Sidoni, kwa mikono ya wajumbe watakaofika Yerusalemu kwa Sedekia, mfalme wa Yuda.
useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee Sidoni, nami natukuzwa kati yako; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapokuwa nimetekeleza hukumu zangu ndani yake, na kutakasika ndani yake.
BWANA akawatia mkononi mwa Israeli, nao wakawapiga, na kuwafukuza mpaka kufikia Sidoni ulio mkuu, tena hadi kufika Misrefoth-maimu, tena hata kufikia bonde la Mispa upande wa mashariki; wakawaua wote, wasibakize hata mtu mmoja
wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi haitasikika ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.
Kisha wana wa Israeli walifanya tena yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA, wakawatumikia Mabaali, na Maashtorethi, na miungu ya Shamu, na miungu ya Sidoni, na miungu ya Moabu, na miungu ya wana wa Amoni, na miungu ya Wafilisti; nao wakamuacha BWANA, wala hawakumtumikia yeye.