Isaya 23:2 - Swahili Revised Union Version Tulieni, enyi mkaao kisiwani; wewe ambaye wafanya biashara wa Sidoni, wavukao bahari, walikujaza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyamazeni kwa mshangao enyi wakazi wa pwani, naam, tulieni enyi wafanyabiashara wa Sidoni, ambao wajumbe wenu wanapita baharini, Biblia Habari Njema - BHND Nyamazeni kwa mshangao enyi wakazi wa pwani, naam, tulieni enyi wafanyabiashara wa Sidoni, ambao wajumbe wenu wanapita baharini, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyamazeni kwa mshangao enyi wakazi wa pwani, naam, tulieni enyi wafanyabiashara wa Sidoni, ambao wajumbe wenu wanapita baharini, Neno: Bibilia Takatifu Nyamazeni kimya, enyi watu wa kisiwani, pia ninyi wafanyabiashara wa Sidoni, ambao mabaharia wamewatajirisha. Neno: Maandiko Matakatifu Nyamazeni kimya, enyi watu wa kisiwani, pia ninyi wafanyabiashara wa Sidoni, ambao mabaharia wamewatajirisha. BIBLIA KISWAHILI Tulieni, enyi mkaao kisiwani; wewe ambaye wafanya biashara wa Sidoni, wavukao bahari, walikujaza. |
Nyamazeni mbele zangu, enyi visiwa, na mataifa wajipatie nguvu mpya; na waje karibu wakanene; na tukaribiane pamoja kwa hukumu.
Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu.
Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.