Isaya 2:5 - Swahili Revised Union Version Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sasa, enyi wazawa wa Yakobo, njoni, tutembee katika mwanga wa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Sasa, enyi wazawa wa Yakobo, njoni, tutembee katika mwanga wa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sasa, enyi wazawa wa Yakobo, njoni, tutembee katika mwanga wa Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Njooni, enyi nyumba ya Yakobo, tutembeeni katika nuru ya Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Njooni, enyi nyumba ya Yakobo, tutembeeni katika nuru ya bwana BIBLIA KISWAHILI Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya BWANA. |
Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu.
Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubirie watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.
Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.
Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; nendeni kama watoto wa nuru,
Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lolote hamna ndani yake.
bali tukienenda katika nuru, kama yeye alivyo katika nuru, tunashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.