Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao; Wanafurahi mbele zako, Kama furaha ya wakati wa mavuno, Kama watu wafurahivyo wagawanyapo nyara.
Isaya 16:9 - Swahili Revised Union Version Basi, naililia mizabibu ya Sibma kwa kilio cha Yazeri, nitawanyeshea machozi yangu, Ee Heshboni na Eleale, kwa kuwa kelele za vita zimeyaangukia mavuno ya matunda yako, na mavuno ya mizabibu yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo ninalia pamoja na Yazeri kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Machozi yananitoka kwa ajili yenu, enyi miji ya Heshboni na Eleale; maana vigelegele vya mavuno ya matunda, vigelegele vya mavuno ya nafaka vimetoweka. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo ninalia pamoja na Yazeri kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Machozi yananitoka kwa ajili yenu, enyi miji ya Heshboni na Eleale; maana vigelegele vya mavuno ya matunda, vigelegele vya mavuno ya nafaka vimetoweka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo ninalia pamoja na Yazeri kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Machozi yananitoka kwa ajili yenu, enyi miji ya Heshboni na Eleale; maana vigelegele vya mavuno ya matunda, vigelegele vya mavuno ya nafaka vimetoweka. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo, kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Ee Heshboni, ee Eleale, ninakulowesha kwa machozi! Shangwe za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo, kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Ee Heshboni, ee Eleale, ninakulowesha kwa machozi! Kelele za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa. BIBLIA KISWAHILI Basi, naililia mizabibu ya Sibma kwa kilio cha Yazeri, nitawanyeshea machozi yangu, Ee Heshboni na Eleale, kwa kuwa kelele za vita zimeyaangukia mavuno ya matunda yako, na mavuno ya mizabibu yako. |
Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao; Wanafurahi mbele zako, Kama furaha ya wakati wa mavuno, Kama watu wafurahivyo wagawanyapo nyara.
Na mimi, tazama, nitakaa Mizpa, ili nisimame mbele ya Wakaldayo watakaotujia; lakini ninyi chumeni divai, na matunda ya wakati wa jua, na mafuta, mkaviweke vitu hivyo katika vyombo vyenu, mkakae katika miji yenu mliyoitwaa.
basi, Wayahudi wote wakarudi kutoka kila mahali walikofukuzwa wakaenda mpaka nchi ya Yuda, wakamwendea Gedalia huko Mizpa, wakakusanya divai, na matunda ya wakati wa jua mengi sana.
nao watajifanya kuwa na upaa kwa ajili yako, na kujifunga nguo za magunia viunoni, nao watakulilia kwa uchungu wa roho, kwa maombolezo ya uchungu.
Mwanadamu, walilie watu wa Misri. Wote jamii ukawabwage, naam, yeye, na binti za mataifa mashuhuri, hata pande za chini za nchi, pamoja na watu washukao shimoni.
Nao wakatoka kwenda mashambani, wakavuna mashamba yao ya mizabibu, na kuzishindika hizo zabibu, na kufanya sikukuu, kisha wakaingia nyumbani mwa mungu wao, wakala na kunywa na kumlaani huyo Abimeleki.