wakasema, BWANA alimwagiza bwana wangu awape wana wa Israeli nchi kwa kupiga kura iwe urithi wao; tena bwana wangu aliagizwa na BWANA awape binti za Selofehadi ndugu yetu huo urithi wa baba yao.
Hesabu 36:3 - Swahili Revised Union Version Wakiolewa na watu wa wana wa hayo makabila mengine ya wana wa Israeli, ndipo urithi wao utatwaliwa na kuondolewa katika urithi wa baba zetu, na hilo kabila watakalotiwa ndani yake litaongezewa urithi wao; basi urithi huo utaondolewa katika kura ya urithi wetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini wao wakiolewa na Waisraeli wa makabila mengine, urithi wao utatoka kwetu na kuwaendea watu wa kabila watakamoolewa; kwa hiyo urithi wetu sisi utapungua. Biblia Habari Njema - BHND Lakini wao wakiolewa na Waisraeli wa makabila mengine, urithi wao utatoka kwetu na kuwaendea watu wa kabila watakamoolewa; kwa hiyo urithi wetu sisi utapungua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini wao wakiolewa na Waisraeli wa makabila mengine, urithi wao utatoka kwetu na kuwaendea watu wa kabila watakamoolewa; kwa hiyo urithi wetu sisi utapungua. Neno: Bibilia Takatifu Sasa ikiwa wataolewa na wanaume wa makabila mengine ya Israeli, itakuwa kwamba urithi wao utaondolewa kutoka urithi wa mababu zetu na kuongezwa katika urithi wa kabila ambalo dada hao wameolewa. Kwa hiyo sehemu ya urithi tuliyogawiwa itachukuliwa kutoka kwetu. Neno: Maandiko Matakatifu Sasa ikiwa wataolewa na watu wa makabila mengine ya Kiisraeli, itakuwa kwamba urithi wao utaondolewa kutoka urithi wa mababu zetu na kuongezwa katika urithi wa kabila ambalo dada hao wameolewa. Kwa hiyo sehemu ya urithi tuliyogawiwa itachukuliwa kutoka kwetu. BIBLIA KISWAHILI Wakiolewa na watu wa wana wa hayo makabila mengine ya wana wa Israeli, ndipo urithi wao utatwaliwa na kuondolewa katika urithi wa baba zetu, na hilo kabila watakalotiwa ndani yake litaongezewa urithi wao; basi urithi huo utaondolewa katika kura ya urithi wetu. |
wakasema, BWANA alimwagiza bwana wangu awape wana wa Israeli nchi kwa kupiga kura iwe urithi wao; tena bwana wangu aliagizwa na BWANA awape binti za Selofehadi ndugu yetu huo urithi wa baba yao.
Tena itakapokuwapo hiyo jubilii ya wana wa Israeli, ndipo urithi wa hilo kabila ambalo wamekuwa ndani yake utaongezewa huo urithi wao; hivyo urithi wao utaondolewa katika urithi wa kabila la baba zetu.