Hesabu 33:7 - Swahili Revised Union Version Wakasafiri kutoka Ethamu, na kurudi nyuma hata Pi-hahirothi palipokabili Baal-sefoni; wakapiga kambi mbele ya Migdoli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kutoka Ethamu, waligeuka na kurudi hadi Pi-hahirothi, mashariki ya Baal-sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli. Biblia Habari Njema - BHND Kutoka Ethamu, waligeuka na kurudi hadi Pi-hahirothi, mashariki ya Baal-sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kutoka Ethamu, waligeuka na kurudi hadi Pi-hahirothi, mashariki ya Baal-sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli. Neno: Bibilia Takatifu Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki mwa Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli. Neno: Maandiko Matakatifu Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli. BIBLIA KISWAHILI Wakasafiri kutoka Ethamu, na kurudi nyuma hata Pi-hahirothi palipokabili Baal-sefoni; wakapiga kambi mbele ya Migdoli. |
Waambie wana wa Israeli, kwamba warudi na kupiga kambi yao mbele ya Pi-hahirothi, kati ya Migdoli na bahari, kukabili Baal-sefoni; mtapanga mbele yake karibu na bahari.
Wamisri wakafuata nyuma yao, farasi wote na magari yote ya Farao, na askari zake wenye kupanda farasi, na jeshi lake, nao wakawapata wakiwa wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni.
Wakasafiri kutoka hapo mbele ya Hahirothi, wakapita katikati ya bahari na kuingia jangwani; kisha wakaenda safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu, wakapiga kambi Mara.