BWANA akamwambia Musa, Mtwae Yoshua, mwana wa Nuni, mtu ambaye roho iko ndani yake, ukamwekee mkono wako;
Hesabu 27:23 - Swahili Revised Union Version kisha akaweka mikono yake juu yake, akampa mausia, kama BWANA alivyosema kwa mkono wa Musa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha akamwekea mikono kichwani na kumpa mamlaka kama alivyoagizwa na Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Kisha akamwekea mikono kichwani na kumpa mamlaka kama alivyoagizwa na Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha akamwekea mikono kichwani na kumpa mamlaka kama alivyoagizwa na Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Kisha akaweka mikono yake juu ya kichwa cha Yoshua na kumpa maagizo, kama vile Mwenyezi Mungu alivyoelekeza kupitia kwa Musa. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha akaweka mikono yake juu ya kichwa cha Yoshua na kumpa maagizo, kama vile bwana alivyoelekeza kupitia kwa Musa. BIBLIA KISWAHILI kisha akaweka mikono yake juu yake, akampa mausia, kama BWANA alivyosema kwa mkono wa Musa. |
BWANA akamwambia Musa, Mtwae Yoshua, mwana wa Nuni, mtu ambaye roho iko ndani yake, ukamwekee mkono wako;
kisha ukamweke mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya jumuiya yote; ukampe mausia mbele ya macho yao.
Musa akafanya kama BWANA alivyomwamuru; akamtwaa Yoshua, akamweka mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya jumuiya yote;
Nikamwamuru Yoshua wakati huo, nikamwambia, Macho yako yameona yote aliyowatenda BWANA, Mungu wenu, wale wafalme wawili, navyo ndivyo atakavyoutenda BWANA kila ufalme huko uvukiako.
Lakini mwagize Yoshua, mtie moyo na nguvu, umtie na nguvu; kwani ndiye atakayevuka mbele ya watu hawa, na nchi utakayoiona atawarithisha yeye.
Akamwagiza Yoshua, mwana wa Nuni, akamwambia, Uwe hodari na moyo mkuu, kwa kuwa utawapeleka wana wa Israeli katika nchi niliyowaapia; nami nitakuwa pamoja nawe.
Na Yoshua, mwana wa Nuni, alikuwa amejaa roho ya hekima; maana Musa alikuwa amemwekea mikono yake juu yake; wana wa Israeli wakamsikiliza, wakafanya kama BWANA alivyomwamuru Musa.