Hesabu 20:25 - Swahili Revised Union Version Uwatwae Haruni na mwanawe Eleazari uwalete juu ya mlima wa Hori; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mchukue Aroni na Eleazari mwanawe, uwalete juu ya Mlima Hori. Biblia Habari Njema - BHND Mchukue Aroni na Eleazari mwanawe, uwalete juu ya Mlima Hori. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mchukue Aroni na Eleazari mwanawe, uwalete juu ya Mlima Hori. Neno: Bibilia Takatifu Watwae Haruni na Eleazari mwanawe, na uwapandishe juu katika Mlima Hori. Neno: Maandiko Matakatifu Watwae Haruni na Eleazari mwanawe, na uwapandishe juu katika Mlima wa Hori. BIBLIA KISWAHILI Uwatwae Haruni na mwanawe Eleazari uwalete juu ya mlima wa Hori; |
Kisha Musa akamwambia Haruni na wanawe Eleazari na Ithamari, Msiache wazi nywele za vichwani mwenu, wala msiyararue mavazi yenu; ili kwamba msife, tena asiukasirikie mkutano wote; lakini ndugu zenu, nyumba yote ya Israeli, na waomboleze kwa ajili ya waliochomwa na moto wa BWANA.
Kisha Nadabu na Abihu walikufa mbele za BWANA, waliposongeza moto wa kigeni mbele za BWANA, katika jangwa la Sinai, nao walikuwa hawana wana; na Eleazari na Ithamari wakafanya kazi ya ukuhani wakati wa uhai wa Haruni baba yao.
(Wana wa Israeli wakasafiri kutoka visima vya Bene-yaakani kwenda Mosera; Haruni akafa huko, akazikwa huko; na Eleazari mwanawe akahudumu kama kuhani badala yake.