Wataila sadaka ya unga, na sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia, na kila kitu katika Israeli kilichowekwa wakfu kitakuwa chao.
Hesabu 18:14 - Swahili Revised Union Version Kila kitu kilichowekwa wakfu katika Israeli kitakuwa chako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila kitu kilichowekwa wakfu nchini Israeli kitakuwa chenu. Biblia Habari Njema - BHND Kila kitu kilichowekwa wakfu nchini Israeli kitakuwa chenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila kitu kilichowekwa wakfu nchini Israeli kitakuwa chenu. Neno: Bibilia Takatifu “Kila kitu katika Israeli ambacho kimetolewa kwa Mwenyezi Mungu ni chenu. Neno: Maandiko Matakatifu “Kila kitu katika Israeli ambacho kimetolewa kwa bwana ni chenu. BIBLIA KISWAHILI Kila kitu kilichowekwa wakfu katika Israeli kitakuwa chako. |
Wataila sadaka ya unga, na sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia, na kila kitu katika Israeli kilichowekwa wakfu kitakuwa chao.
ila hilo shamba litakuwa takatifu kwa BWANA litakapotoka katika jubilii, kama ni shamba lililowekwa wakfu; litakuwa mali ya kuhani.
Pamoja na hayo, hakitauzwa wala kukombolewa kitu chochote kilichowekwa wakfu, ambacho mtu amekiweka wakfu kwa BWANA, katika vitu vyote alivyo navyo, kama ni mtu, au mnyama, au kama ni shamba la milki yake; kila kitu kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa BWANA.