Basi wakasafiri kutoka penye mlima wa BWANA safari ya siku tatu; na sanduku la Agano la BWANA likatangulia mbele yao mwendo wa siku tatu, ili kuwatafutia mahali pa kupumzika.
Hesabu 14:44 - Swahili Revised Union Version Lakini walithubutu kukwea mlimani hata kileleni; ila sanduku la Agano la BWANA halikutoka humo kambini, wala Musa hakutoka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata hivyo, wao walisisitiza kwenda juu milimani, ingawa sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, wala Mose hakuondoka kambini. Biblia Habari Njema - BHND Hata hivyo, wao walisisitiza kwenda juu milimani, ingawa sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, wala Mose hakuondoka kambini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata hivyo, wao walisisitiza kwenda juu milimani, ingawa sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, wala Mose hakuondoka kambini. Neno: Bibilia Takatifu Hata hivyo, kwa kiburi chao walipanda juu kuelekea nchi ya vilima virefu, ijapokuwa Musa hakutoka kambini wala Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Hata hivyo, kwa kiburi chao walipanda juu kuelekea nchi ya vilima virefu, ijapokuwa Musa hakutoka kambini wala Sanduku la Agano la bwana. BIBLIA KISWAHILI Lakini walithubutu kukwea mlimani hata kileleni; ila sanduku la Agano la BWANA halikutoka humo kambini, wala Musa hakutoka. |
Basi wakasafiri kutoka penye mlima wa BWANA safari ya siku tatu; na sanduku la Agano la BWANA likatangulia mbele yao mwendo wa siku tatu, ili kuwatafutia mahali pa kupumzika.
Kwa kuwa Mwamaleki na Mkanaani wako mbele yenu, nanyi mtaanguka kwa upanga, kwa sababu mmerudi nyuma msimfuate BWANA, kwa hiyo BWANA hatakuwa pamoja nanyi.
Lakini mtu afanyaye neno lolote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana BWANA; na mtu huyo atatupiliwa mbali na watu wake.
Basi Musa akawatuma watu elfu wa kila kabila waende vitani, wao na Finehasi mwana wa Eleazari kuhani, waende vitani, na vile vyombo vya mahali patakatifu, na hizo tarumbeta za kupiga sauti za kugutusha mkononi mwake.
Hata ingawa niliwaambia, hamkunisikiza, bali mliasi amri ya Bwana, makajiamini na kulewa mlimani.