Hesabu 11:19 - Swahili Revised Union Version Hamtakula siku moja, wala siku mbili, wala siku tano, wala siku kumi, wala siku ishirini; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtakula nyama si kwa muda wa siku moja tu, au mbili, au tano, au kumi au ishirini, Biblia Habari Njema - BHND Mtakula nyama si kwa muda wa siku moja tu, au mbili, au tano, au kumi au ishirini, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtakula nyama si kwa muda wa siku moja tu, au mbili, au tano, au kumi au ishirini, Neno: Bibilia Takatifu Hamtaila kwa siku moja tu, au siku mbili, au tano, kumi au siku ishirini, Neno: Maandiko Matakatifu Hamtaila kwa siku moja tu, au siku mbili, au tano, kumi au siku ishirini, BIBLIA KISWAHILI Hamtakula siku moja, wala siku mbili, wala siku tano, wala siku kumi, wala siku ishirini; |
Kisha uwaambie watu hawa, Jitakaseni nafsi zenu kabla ya kesho, nanyi mtakula nyama; kwa maana mmelia masikioni mwa BWANA, mkisema, Ni nani atakayetupa nyama, tule? Maana huko Misri tulikuwa na uheri. Basi kwa sababu hiyo BWANA atawapa nyama, nanyi mtakula.
lakini mtakula muda wa mwezi mzima, hadi hapo nyama hiyo itakapotoka katika mianzi ya pua zenu, nanyi mtaikinai, kwa sababu mmemkataa BWANA aliye kati yenu, na kulia mbele zake, mkisema, Tulitoka Misri kwa maana gani?